Twaweza.org

Watoto wetu wanajifunza? Tathmini ya Uwezo Tanzania 2012

Wakati ambapo asilimia 100 ya watoto wa Darasa la 3 na kuendelea wanapaswa kuweza kusoma na kufanya hesabu za kiwango fulani, matokeo ya Uwezo yanaonyesha kwamba ni wachache tu ndiyo wanaoweza kufanya hivyo. Katika Darasa la 3, mmoja kati ya watoto wanne anaweza kusoma Kiswahili kwa kiwango sahihi. Shule za binafsi zinafanya vizuri zaidi kidogo kulinganisha na zile za Serikali, ambapo asilimia 61 ya watoto walio na umri chini ya miaka 9 hawawezi kusoma Kiswahili na kufanya Hesabu za Kuzidisha kulinganisha na asilimia 85 ya wenzao walio katika shule za Serikali.

Matokeo haya yalitangazwa na Twaweza, inayosimamia Tafiti ya Uwezo, katika ripoti yake ya tatu ya Tathmini ya Mwaka ya Ujifunzaji. Matokeo haya yamejikita zaidi kwenye tathmini kubwa kabisa ya mwaka kwa ngazi ya kaya inayopima stadi za kusoma na kufanya hesabu za msingi za watoto. Tathmini ilifanyika nchi nzima mwaka 2012; ikipima watoto 104,568 wenye umri kati ya miaka 7 hadi 16 katika kaya 55,191, katika maeneo (vijiji) 3,752, kwenye wilaya 126 za Tanzania.

Tathmini ya Uwezo inaonyesha kwamba utendaji uko duni nchini kote. Matokeo muhimu yalikuwa:

Mtoto mmoja tu kati ya watoto wanne wa Darasa la Tatu anaweza kusoma hadithi ya Darasa la Pili kwa Kiswahili.

Watoto wanne kati ya kumi wa Darasa la Tatu wanaweza kuzidisha hesabu ngazi ya Darasa la Pili

Mtoto moja kati ya kumi wa Darasa la Tatu anaweza kusoma hadithi ya ngazi ya Darasa la Pili kwa Kiingereza.

Mahali mtoto anaishi panaweza kuathiri uwezo wake wa kusoma na hesabu.

Kwa wastani, watoto saba kati ya kumi hawajui maana ya rangi tatu za Bendera ya Taifa.

Endelea kusoma:

Authors: Sam Jones

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri