Twaweza.org

Uwezo Yatoa Ripoti ya Afrika Mashariki

Ripoti ya Uwezo ya Afrika Mashariki, 2011, kwa mara ya kwanza, inaonesha takwimu ambazo zinalinganisha kiwango cha ufahamu wa Kiingereza na Kiswahili na ujuzi wa Hesabu kwa nchi za Afrika Mashariki. Ripoti inatokana na taftishi iliyohusisha zaidi ya kaya 80,000—zoezi kubwa la aina yake. Matokeo yanatoa picha halisi tuliyonayo hadi hivi sasa kuhusu msingi walionao raia wa Kenya, Uganda na Tanzania kuwawezesha kustawi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Je kila nchi imefaulu vipi kwa kuzingatia vigezo ilivyojiwekea? Je ufaulu wake unalinganaje na wa nchi jirani. Na je tunapata picha gani tukiangalia takwimu kwa kulinganisha makundi ya kaya zenye vipato tofauti? Sababu zipi zinachochea mafanikio? Ripoti hii inajibu maswali haya. Isome hapa.

Endelea kusoma: basic education East Africa

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri