Twaweza.org

Vyombo vya habari Afrika Mashariki vyaandika kuhusu Ushirikiano wa Serikali Zilizo Uwazi

Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi (Open Government Partnership-OGP) ulizinduliwa rasmi jijini New York, 20 Septemba 2011 na Rais Barack Obama katika hafla iliyofanyika wakati wa Mkutano wa 66 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa. Wawakilishi toka nchi 40 walihudhuria uzinduzi wa OGP, wakiwamo Mwai Kibaki wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania. Nchi hizi mbili ni mojawapo ya tano tu za Afrika ambazo zimeshahakikisha utashi wao kujiunga na OGP na sasa zinaandaa mipango kazi ya nchi zao. Kiongozi wa Twaweza,  Rakesh Rajani, alikuwapo kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Asasi Zisizo za Kiserikali. Katika hotuba kuhitimisha tukio hilo Rais Obama alisisitiza mchango wa uwajibikaji unaoendeshwa na raia na akarejea kipekee hotuba ya Rakesh Rajani.

Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi ni jitihada mpya ya kimataifa yenye lengo la kuibua utashi madhubuti kwa serikali kuchochea uwazi, kuwawezesha raia, kupambana na rushwa na kutumia technolojia mpya kuboresha serikalini. Katika muktadha wa ushirikano baina ya wadau wengi, serikali na mashirika ya kiraia yameungana kuunda Kamati Tendaji ya OGP.

Ili kujiunga na OGP, nchi washiriki lazima kwanza kutekeleza Azimio la Serikali Wazi. Nchi wanachama zinatakiwa kukamilisha mpango kazi wa taifa unaoandaliwa kwa kushirikisha umma; na pia nchi wanachama zapaswa kuruhusu uchunguzi huru wa hatua wanazopiga .

Uzinduzi wa OGP ulifuatiliwa kwa makini na vyombo vya habari duniani kote. Gazeti la Wall Street Journal lilichapa picha ya ukurasa wa mbele toka kwenye tukio hilo. East African lilichapa makala mbili kuhusu OGP na kuchapa makala zifuatazo:Serikali zinazoshirikisha raia ndio zitafanikiwa, na Marekani yaipongeza Kenya na Tanzania, na makala ya kihariri kuhusu OGP.

Katika hotuba yake ya mwisho wa Mwezi Septemba 2011 Rais Kikwete wa Tanzania alizungumzia pia OGP. Habari Leo, liliandika likizungumzia kipengele cha OGP kama kilivyojitokeza kwenye hotuba ya rais.  

Kufuatia hayo, Twaweza, kwa kuitikia wito wa Rais Kikwete, imetoa maelezo kuhusu Ushirikiano wa Serikali Huru kwa maofisa wa ngazi ya juu wa Serikali Ikulu, kwa Makatibu Wakuu, na inatarajiwa kulieleza Baraza la Mawaziri kabla ya mwisho wa Oktoba 2011. Twaweza itasaidiana na Serikali kupata maoni ya umma na kuandaa mpango wa awali wa utekelezaji wa kanuni za Serikali Wazi nchini Tanzania.

Endelea kusoma: katika vyombo vya habari

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri