Twaweza.org

Walimu wakuu waadibishwa kwa matokeo mabaya ya mitihani

Katika wilaya moja nchini Uganda, walimu wakuu wameadibishwa na mamlaka za elimu kwa ufaulu mdogo wa wanafunzi katika mitihani ya kumaliza elimu ya msingi mwaka 2011. New Vision linaripoti kuwa kati ya shule 121 zinazoendeshwa na Serikali katika wilaya  ya Hoima ni 23 tu ndio zina angalau mwanafunzi mmoja aliyepata alama za daraja la kwanza. Maafisa Elimu wa wilaya ya Hoima wanasema watatuma barua ya onyo kwa walimu wakuu wote wa shule ambazo hazina wanafunzi waliopata daraja la kwanza. Iwapo hakutatakuwa na mabadiliko katika mitihani ijayo walimu wakuuu wanaweza kufukuzwa kazi.

Walimu wakuu katika wilaya hiyo wanasema pamoja na juhuzi zao kubwa, kuna mazingira ambayo ni juu ya uwezo wao. Wanakabiliana na upungufu wa waalimu na mishahara midogo kwa walimu waliopoa, madarasa yaliyofurika wanafunzi, uhaba wa miundombinu na vifaa.

Utafiti wa upimaji wa kujifunza wa Uwezo 2011 ulibaini ujifunzaji haba katika kusoma na kuandika kati ya watoto wa umri wa shule ya msingi nchini Uganda. Soma zaidi.

Endelea kusoma: basic education uganda

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri