Elimu

< iliyopita 1 ifuatayo >
6 makala
Sort by: Maoni |

Hali Halisi

Benki ya taarifa 29 Nov 2016 | Elimu

Maoni ya wananchi kuhusu hali ya elimu nchini Tanzania ndani ya mwaka mmoja uliopita; hasa juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu kwa kuongeza madawati, elimu bila malipo na ruzuku zinazotumwa moja kwa moja mashuleni.

Ufunguo wa maisha?

Benki ya taarifa 16 Jul 2016 | Elimu

Katika muhutasari huu, tunatoa taarifa juu ya mawazo ya wananchi juu ya elimu, na hasa ubora wa elimu ya sekondari.

Mwanga Mpya?

Benki ya taarifa 25 Feb 2016 | Elimu

Maoni ya wananchi kuhusu mabadiliko kwenye sekta ya elimu

Nini kinaendelea kwenye shule zetu?

Benki ya taarifa 30 Jun 2014 | Elimu

Mwananchi 1 tu kati ya 10 ndiye anayefikiri kuwa watoto wengi wanaomaliza darasa la 2 wana uwezo wa kusoma na kufanya hisabati wa darasa hilo hilo (ngazi ya darasa la 2). Mbaya zaidi, wananchi 3 tu kati ya 10 (31%) wanafikiri kuwa watoto hawa wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma na kuhesabu kwenye ngazi yao; ikimaanisha kuwa wananchi hawana matumaini kama kweli mfumo wa elimu utawafundisha watoto ujuzi na stadi wanazotakiwa kupata wakiwa shuleni.Muhtasari huu unachunguza hali ya shule zetu, ufundishaji na ujifunzaji pamoja na ushiriki wa wazazi kwenye elimu ya watoto wao.

Sauti za Wananchi, Fedha za Ruzuku

Benki ya taarifa 1 Aug 2013 | Elimu

Kiasi cha fedha za ruzuku kilichopokelewa katika robo ya kwanza tu ya mwaka 2013 kinaripotiwa kuwa karibu sawa na wastani uliogawiwa kwa mwaka mzima katika miaka mitatu iliyopita. Hata hivyo, wazazi wanashindwa kufuatilia kuhusu fedha hizi kwani 8 kati ya 10 hawajui ni kiasi gani cha fedha za ruzuku kinapaswa kutolewa kwa kila mwaka.

Sauti za Wananchi, Matokeo ya Kidato cha Nne

Benki ya taarifa 14 May 2013 | Elimu

Wazazi wana ufahamu kuhusu mwendelezo wa kuanguka kwa ubora wa elimu ya sekondari, na kwa kiasi kikubwa wanatupa lawama kwa serikali na walimu kwa kuanguka huko. Matokeo haya yamechapishwa katika muhtasari wa Twaweza unaoitwa Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne: Wananchi wazungumzia mgogoro wa kujifunza Tanzania. Muhtasari huo umeandaliwa kutokana na takwimu zilizokusanywa kupitia utafiti wa Sauti za Wananchi, ambao ni utafiti wa njia ya simu za mkononi wenye sura ya uwakilishi wa kaya kitaifa kote Tanzania Bara.

< iliyopita 1 ifuatayo >
6 makala
Sort by: Maoni |