Twaweza.org

Kulinda haki za kila mtu: Maoni ya wananchi juu ya ulemavu

Karibu nusu ya wananchi (46%) wameripoti kuwahi kushuhudia ubaguzi  dhidi ya watu wenye ulemavu katika ajira. Wakati huo huo, ni wananchi wawili tu kati ya kumi (17%) waliokiri kufahamu asasi/mashirika yanayotoa upendeleo kwenye suala la kuwaajiri watu wenye ulemavu. Wananchi waliripoti kuwa miongoni mwa mashirika haya asilimia 38 ni taasisi za kiserikali. Vile vile wananchi waliripoti kuwafahamu watoto wenye umri wa kwenda shule ambao ni walemavu ila hawakuwa shuleni. Mwananchi mmoja kati ya watatu alisema anamfahamu mtoto mwenye umri wa kusoma shule ya msingi, na wawili kati ya kumi waliwajua watoto wenye umri wa kusoma shule ya sekondari lakini hawakuwa shule.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Kulinda haki za kila mtu: Maoni ya wananchi juu ya ulemavu. Muhtasari huu umetokana na Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kupitia simu ya mkononi. Utafiti huu hukusanya taarifa kwenye kaya zote Tanzania Bara. Takwimu zilikusanywa mwezi Julai 2014.

Matokeo haya yameyotokana na mitazamo ya wananchi yanayoibua kwa undani ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu ama moja kwa moja au kwa kupitia kukosekana kwa huduma na ajira.

Wananchi walikuwa na mtazamo ulioonesha kuwa wanawajali watu wenye ulemavu. Idadi kubwa ya wananchi (91%) waliripoti kuwa wanawaona watu wenye ulemavu kama watu wanaohitaji kutunzwa. Vile vile mwananchi mmoja kati ya watatu aliripoti kuwaona watu wenye ulemavu kama siyo watu kamili (33%) au kuwa ni watu ambao ni kikwazo kwao (32%). Karibu nusu ya wahojiwa (46%) wanawaona watu wenye ulemavu kama mzigo kiuchumi kwa familia zao na ni wananchi wanne kati ya kumi (39%) wanaowaona kama watu wenye uzalishaji mdogo kuliko watu wasio na ulemavu.
 

Endelea kusoma:

Authors: Angela Ambroz

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri