Twaweza.org

Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye?

Zaidi ya nusu ya wananchi (54%) wanafikiri kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi ifikapo mwaka 2025. Huu ndio mtazamo wa wananchi wakio katika makundi yote- vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, na wakazi wa vijijini na mijini. Mtazamo huu ni tofauti kabisa na ule wa nchi za Marekani na Ulaya ambapo karibu wananchi saba kati ya kumi (65%) wanafikiri kuwa watoto wao watakuwa na hali mbaya zaidi kifedha kuliko walivyo wao sasa.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza na Society for International Development (SID) kwenye muhtasari wa utafiti wenye jina la Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye? Muhtasari umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika kwa njia ya simu za mkononi. Utafiti huu hufanyika katika maeneo yote Tanzania Bara (Zanzibar haimo kwenye matokeo haya). Matokeo haya yametokana na takwimu zilizokusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,408 mwezi Agosti 2014.

Wakiangalia nchi kwa ujumla, wananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa Tanzania itakuwa mahali pazuri pa kuishi mwaka 2025. Wananchi makundi yote bila kujali hali zao za kiuchumi wanaamini hivyo; mathalan, wananchi wenye kipato kikubwa 64% na wananchi maskini 68% wana matumaini na siku zijazo. Watanzania wana matumaini na akiba tuliyonayo kwa ajili ya nchi.

Hata hivyo, baadhi ya wananchi bado wana wasiwasi. Karibu mwananchi mmoja kati ya watano (18%) wanahofia maisha yako yatakuwa mabaya zaidi mwaka 2025 kuliko yalivyo leo, na wapo wengine wanaodhani nchi itakuwa mahali pabaya pa kuishi mwaka 2025. Hapa kuna baadhi ya tofauti kati ya matajiri na maskini, mwananchi mmoja kati ya wanne katika kundi la matajiri (25%) na mmoja kati ya watano katika kundi la maskini (18%) hawana matumaini kuhusu siku zijazo.
 

Endelea kusoma:

Authors: Aidan Eyakuze

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri