Twaweza.org

Usalama Wetu? Maoni ya wananchi juu ya usalama na haki

Wananchi watatu kati ya kumi (30%) wameshakukumbana na wizi ndani ya kipindi cha mwaka jana. Kwa ujumla, nusu ya Watanzania wote wamewahi kuibiwa.

Ailimia 84 ya wananchi wanaamini kuwa kuna uwezekano wa wao kuathiriwa na makundi ya vijana wahalifu kama Panya Road. Mwezi Januari 2015, Panya Road ilileta wasiwasi mkubwa jijini Dar es Salaam kwa kufanya vitendo vya uhalifu na vurugu, tukio hili lilitawala mijadala kwenye mitandao ya kijamii na kupelekea mamia ya vijana hao kukamatwa. Wananchi sita kati ya kumi (60%) kitaifa wamewahi kusikia kuhusu Panya Road lakini karibu wananchi tisa kati ya kumi (87%) walisema hakuna kikundi kama hicho katika maeneo yao.

Wananchi wawili kati ya kumi (18%) wameripoti kuwa walishuhudia ghasia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa mwezi Desemba 2014.

Matokeo haya yametolewa na Twaweza kwenye muhtasari wake wa utafiti wenye jina la Je, tuko Salama? Maoni ya wananchi juu ya usalama na haki. Muhtasari huu umetokana na takwimu za Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu ya mkononi. Takwimu hizi zilikusanywa kwa wahojiwa 1,401 kutoka Tanzania Bara (Zanzibar haimo katika matokeo haya) mwezi Februari na Machi 2015.
 

Endelea kusoma:

Authors: Angela Ambroz

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri