Twaweza.org

Ufunguo wa maisha | Maoni ya wananchi juu ya umuhimu wa shule Muhtasari huu

Nchini Tanzania, shilingi 25 kati ya 100 zinatengwa na serikali kwa ajili ya elimu. Licha ya hilo, mtoto mmoja kati ya watatu humaliza elimu ya msingi bila kujua kusoma na kuhesabu.

Sera mpya ya elimu imezinduliwa mwaka huu wa 2015. Elimu ya msingi sasa imepangiliwa kuwa ya miaka kumi badala ya miaka saba. Elimu hii itakuwa ni ya lazima kwa wote na wazazi hawatohitajika kulipa ada. Serikali imeahidi kufuta ada hii kuanzia mwaka 2016.

Hata hivyo, kwa upande wa elimu ya sekondari, ubora wake pia hauridhishi – hii inadhihirishwa na kuendelea kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mitihani ya Taifa. Sera hii mpya ni sehemu ya mkakati wa kujibu malalamiko ya wananchi kulikotokana na matokeo mabaya ya kidato cha 4. Hatua za kuinua ubora wa elimu ya sekondari ni pamoja na kuinua ari ya walimu na kuboresha miundombinu ya elimu.

Je, sera mpya itainua ubora wa kujifunza? Ni kwa kiasi gani inajibu matarajio na matamanio ya mwananchi wa kawaida kwa watoto wake?

Katika muhutasari huu, tunatoa taarifa juu ya mawazo ya wananchi juu ya elimu, na hasa ubora wa elimu ya sekondari. Madodoso yaliyotumika kupata taarifa hii yaliandaliwa kwa ushirikiano na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (WEMU). Takwimu zilikusanywa kati ya tarehe 5 na 22 Novemba 2014 katika sampuli yenye uwakilishi wa kitaifa. Utafiti huu wa Sauti za Wananchi ulifanywa kwa njia ya simu za mkononi. Takwimu zilikusanywa kutoka kwa wahojiwa 1,381, na ni wakilishi kwa Tanzania Bara.

Matokeo muhimu kwenye muhtasari huu ni:

  • Mwananchi mmoja kati ya wawili anaamini kwamba kujua kusoma na kuandika ni stadi muhimu kwa wanaomaliza elimu ya sekondari.
  • Wananchi sita kati ya kumi wanaamini kwamba elimu ya msingi inawaandaa wanafunzi vizuri kuendelea na elimu ya sekondari.
  • Karibu wananchi wawili kati ya watatu wanaamini kuwa watoto wanapaswa kufundishwa kwa lugha ya Kiingereza katika shule za msingi na sekondari.

Endelea kusoma:

Authors: Angela Ambroz

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri