Twaweza.org

Je, watoto wetu wanajifunza?

Licha ya matarijio kuwa watoto wote wa darasa la 3 wangeweza kusoma Kiswahili na Kiingereza, pamoja na kufanya hesabu rahisi za darasa la pili, ripoti mpya ya utafiti inaonesha kuwa ni wanafunzi wachache mno wenye uwezo huo.

Kiswahili
Nusu ya watoto wa darasa la 3 (45%) wanaweza kusoma hadithi ya Kiswahili ya kiwango cha darasa la 2.
Waliofika darasa la 7, ni 4 kati ya 5 (80%) wenye uwezo wa kusoma Kiswahili cha darasa la 2. Hii inaashiria kuwa 20% ya wanafunzi humaliza darasa la 7 wakuwa hawawezi kusoma Kiswahili.

Kiingereza
Wanafunzi 2 kati ya 10 (19%) wa darasa la 3 wanaweza kusoma hadithi ya Kiingereza ya darasa la 2.
Waliofika darasa la 7, ni watoto 6 kati ya 10 (56%) wenye uwezo wa kusoma hadithi ya Kiingereza ya kiwango cha darasa la 2. Takriban nusu ya wanafunzi wote wa darasa la 7 hawajui kusoma Kiingereza, lugha ya kufundishia shule za sekondari.

Hesabu
Watoto 3 kati ya 10 wa darasa la 3 (31%) wanaweza kufanya kwa usahihi hesabu ya kuzidisha za darasa la 2.
Watoto 3 kati ya 10 (29%) wa darasa la 7 hawawezi kufanya hesabu za kuzidisha za darasa la 2.

Matokeo haya yametolewa leo na Uwezo iliyopo Twaweza katika uzinduzi wa ripoti ya utafiti iitwayo Je, Watoto wetu wanajifunza? Uwezo wa Kusoma na kuhesabu nchini Tanzania 2014 (kiingereza). Ripoti hii ni ya nne tangu mwanzo wa tathmini hizi za kila mwaka. Utafiti huu ulifanyika mwaka 2013. Washirika wa Uwezo waliwapima watoto 100,000, wenye umri wa miaka 7-16, kwenye wilaya 131 katika mikoa 25.

Endelea kusoma:

Authors: Uwezo Tanzania

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri