Twaweza.org

Daladala TV

Mvuto wa televisheni katika kukuza fikra na hisia za watazamaji unazidi kukua. Twaweza inafanya kazi na Daladala TV kuanzisha kipindi cha habari za kila siku kikiwa na mkazo katika uchambuzi, mjadala na maongezi miongoni mwa watu wa kawaida kuhusu matukio ya hivi karibuni au mambo yanayoendelea hata wakati huo wa urushaji matangazo. Kipindi hiki kitakuwa ndani ya daladala, basi dogo kama yale yanayotumiwa na Watanzania wengi kwa usafiri wa mijini. Basi hili ni studio ndogo yenye kamera ndogo ndogo na vinasa sauti vilivyopachikwa juu ndani. Mwendesha kipindi atakuwa anaongoza majadiliano kwa kuibua masuala yanayowakereketa wananchi. Kipindi kitakuwa kimeandaliwa kwa kuteua mada mapema, na mada hizo zitakuwa zimefanyiwa utafiti na wahariri. Hii itamwezesha mwendesha kipindi kukiongoza kwa ufanisi na undani unaotakiwa. Kipindi hiki kitaibua sauti ambazo kwa kawaida hazisikiki na kwa njia hii kitawavutia watu ambao kwa kawaida hawavutiwi kuangalia vipindi vya matukio. DalaDala TV itakuwa na vipindi 156 vitakavyokwenda hewani kwa muda wa wiki 26, na kinatarajiwa kuanza mwezi Juni 2010

Endelea kusoma: Televisheni ubia vyombo vya habari

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri