Twaweza.org

Daraja: Kuongeza msukumo wa maji

Daraja ni asasi isiyo ya kiserikali ya Tanzania inayokusudia kutengeneza utaratibu utakaowawezesha wananchi kutoa taarifa kuhusu ufanyaji kazi wa mifumo ya maji katika maeneo husika. Taarifa kutoka kwa wananchi kupitia ujumbe mfupi (sms) au njia nyingine za simu za mkononi zitapokelewa katika kituo cha taarifa (databank) cha sehemu husika, na kituo hicho kitakuwa na ramani ya miundombinu ya maji katika sehemu hiyo.Twaweza inatoa msaada kwa Daraja katika: a) kupeana taarifa zinazoeleweka kuhusu upatikanaji wa huduma ya maji, kimsingi kupitia vyombo vya habari, na b) kuwawezesha wananchi kutoa taarifa kwa muda huohuo kupitia ujumbe mfupi wa simu (sms), na c) kuchambua na kutangaza hatua zinazochukuliwa na serikali kutokana na taarifa hizo za wananchi.

Twaweza itajenga mawasiliano baina ya Daraja na vyombo vya habari na pia viongozi wa madhehebu ya dini kadri kazi hii itakavyoendelea.

Endelea kusoma: maji vijijini Wabia wa Twaweza

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri