Twaweza.org

Uwezo: Kujifunza, siyo tu kujisajili

Twaweza inaunga mkono kazi za Uwezo, harakati inayojikita katika mtazamo wa juhudi za wananchi katika kupima viwango vya uwezo wa kusoma na kuhesabu katika Afrika Mashariki. Uwezo inajishughulisha na upimaji viwango vya ustadi wa kusoma na kufanya mahesabu  miongoni mwa watoto wa miaka kati ya 5-16 katika wilaya zisizopungua asilimia 50 ya wilaya za Afrika Mashariki kupitia tafiti katika ngazi ya kaya (kwa kutumia uzoefu wa ASER nchini India). Mchakato wa tafiti na matokeo yake vinalenga kuwafanya wazazi, wanafunzi, jamii husika na umma kwa ujumla kupata uelewa mkubwa zaidi kuhusu viwango vya kweli vya uwezo wa watoto kusoma, kuandika na kuhesabu. Ziada ya taarifa na uelewa mkubwa zaidi vitasababisha shinikizo kwa ajili ya kuelekeza mjadala wa jamii katika vyombo vya habari na kuzihamasisha serikali ziinue ubora wa elimu kwa kutilia mkazo zaidi katika matokeo ya kujifunza.

Uwezo imehifadhiwa na asasi tatu: TENMET (Mtandao wa Elimu Tanzania); WERK (Wanawake Watafiti wa Elimu Kenya) na UNNGOF (Jukwaa la Asasi zisizo za Kiserikali za Uganda). Tafiti ya kwanza yenye uwakilishi wa kitaifa imekwisha fanyika nchini Kenya na matokeo yake kuwasilishwa kwa umma. Tathimini hii pia imemalizika Uganda na mchakato huu bado unaendelea Tanzania. Uratibu wa kikanda pamoja na ufuatiliaji wa ubora unafanyika kupitia meneja anayefanya kazi katika ofisi za Twaweza jijini Dar es salaam . Ili kupata taarifa zaidi kuhusu programu ya miaka 4 ya Uwezo, soma hapa.

Angalia maelezo (taarifa iko katika lugha ya kiingereza) ya Dk. Sara Ruto wa Uwezo, yaliyowasilishwa makao makuu ya Benki ya Dunia, Washington, tarehe 9 Machi 2010

Endelea kusoma: Elimu Tanzania Ustadi wa kusoma na kuandika Tanzania Uwezo Tanzania Wabia wa Twaweza

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri