Twaweza.org

Matokeo yakipuuzwa, ukaguzi wa nini?

Uwazi, iliyopo Twaweza imetoa muhtasari mpya wa sera unaoitwa, “Matokeo yakipuuzwa, ukaguzi wa nini?” Muhtasari huu unatumia ripoti  za ukaguzi wa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kutathmini mabadiliko katika ubora wa usimamizi wa fedha katika Mamlaka hizo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita. Tathmini inaonesha kwamba viwango vya ubora wa hati  za ukaguzi havikupanda na kwamba hata baada ya miaka mitano ya ukaguzi, usimamizi wa fedha katika Mamlaka nyingi za Serikali za Mitaa bado ni dhaifu. Kwa kiasi kikubwa mapendekezo kutoka kwa Mdhibiti  na Mkaguzi Mkuu wa Serikali yanapuuzwa, na hata hoja za ukaguzi hazifanyiwi kazi.

Muhtasari huu unapendekeza kwamba Tanzania iweke vichocheo vitakavyohakikisha kwamba mapendekezo yanayotokana na ukaguzi yanafanyiwa kazi. Mamlaka inayoteua timu za menejiment  za Mamlaka za Serikali za Mitaa, Wabunge, Kamat  za Uwajibikaji za Bunge, na Wajumbe wa Halmashauri wana wajibu mkubwa kat ka kuhakikisha kwamba jambo hili linafanikiwa. Soma muhtasari mzima.

Endelea kusoma:

Authors: Uwazi

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri