Twaweza.org

Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam:Msongamano wa wanafunzi bila vitabu vya kiada vya kutosha

Uwazi iliyopo Twaweza imetoa muhtasari wa sera kuhusu mazingira ya kusomea kwenye shule za msingi za Serikali za Dar es Salaam. Kwenye muhtasari huu inaripotiwa kuwa pamoja na kuwa karibu na mahali sera zinapotungwa, shule za Dar es Salaam zina mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa na vitabu vya kiada.

Muhtasari huo unaitwa, “Shule za Msingi mkoani Dar es Salaam:Msongamano wa wanafunzi bila vitabu vya kiada vya kutosha.” unaonesha kuwa kwa wastani wanafunzi 81 wanakaa ndani ya darasa ambalo linatarajiwa kuwa na wanafunzi 40. Muhtasari huu unadokeza kuwa karibu nusu ya shule zilizotembelewa wanafunzi wanalazimika kukaa sakafuni kwa kuwa hakuna madawati ya kutosha. Uchambuzi huu umejenjwa kwenye utafiti kwenye sampuli ya shule 40 za msingi za Ilala, Temeke na Kinondoni, na ulifanyika kati ya Agosti na Desemba mwaka 2010. Soma muhtasari mzima.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri