Twaweza.org

Je Watoto Wetu Wanajifunza? Kuhesabu na Kusoma Katika Afrika Mashariki

Ripoti muhimu sana imezinduliwa Jumatatu ya Julai 2 jijini Dar es Salaam. Ripoti ya Uwezo ya Afrika Mashariki, kwa mara ya kwanza ina data zinazolinganisha ujuzi wa Hisabati na Ufahamu kwa Kiswahili na Kiingereza kwa nchi tatu za Afrika Mashariki. Sampuli iliyotumika kwenye utafiti huu, kaya 80,000, ni kubwa ya aina yake. Matokeo ya utafiti huu yanatoa picha halisi ya msingi na utayari wa raia wa Kenya, Uganda na Tanzania kustawi na kushiriki katika Jumuiya ya Afrika Mashariki. Je kila nchi imefanikiwaje kwa kulinganisha na malengo yake husika? Na, kila nchi inafanyaje ikilinganishwa na nyingine? Na je, matokeo yanatoa picha gani pale uchambuzi wa madaraja tofauti ya kipato cha familia yanapochunguzwa? Ni vigezo vipi huleta mafanikio? Ripoti hii inajibu maswali haya na kutoa ufafanuzi zaidi. Isome hapa.

Endelea kusoma:

Authors: Uwazi

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri