Twaweza.org

Sasa ShujaazFM ipo YouTube

ShujaazFM, mradi wa mawasiliano  nchini Kenya na mbia wa Twaweza sasa unarusha matangazo yake kwenye mtandao wa picha za video wa YouTube. Chaneli ya YouTube ya inaongeza kitu kingine bora kwenye mkusanyiko wa mitandao jamii ya ShujaazFM ambapo awali ilikuwapo kwenye Facebook na Twitter.

Gazeti la vichekesho la ShujaazFM ndio chapicho kubwa zaidi nchini Kenya, kilisambaza zaidi ya nakala 600,000 kila mwezi. Kipindi chake cha redio kinarushwa hewani na vituo 20 na maelfu ya mashabiki wanawasiliana kupitia Facebook na Twitter. Washabiki pia wanawasiliana na waigizaji kupitia ujumbe mfupi wa simu na sasa, wanaweza kuwaona nyota wao maarufu kwenye YouTube.

Masuala kuhusu kuongeza kipato na kuepuka shari mitaani yanajadiliwa kwa dakika 5-7 kwenye vipindi vya redio kila siku. Vijana wanapata fursa kuongea, kuwasiliana na kupata taarifa zinazowahusu. Waigizaji wanawatia moyo wasikilizaji kuboresha maisha yao. Mada ni pamoja na mawazo ya kupata fedha na kujiepusha na shari. Fuatilia ShujaazFM YouTube

 

Endelea kusoma: Kenya media shujaazFM youth

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri