Twaweza.org

Wekeni bajeti wazi wa umma, Serikali zaambiwa

DAR ES SALAAM-Tarehe 18 Novemba 2011 karibu makundi 100 ya taasisi za kiraia toka nchi nyingi duniani na mashirika 12 ya kimataifa, yakijumuisha Ushirikiano wa Kimataifa wa Uwazi wa Bajeti, Greenpeace na Kampeni ya ONE, walizindua juhudi za dunia nzima kuchangiza bajeti za Serikali kuwa wazi, shirikishi na zenye kuakisi uwajibikaji. Juhudi hii inajikita katika kujenga muungano wenye nguvu utakaofanya kazi toka mashinani, kitaifa na kimataifa kuhamasisha michakato ya bajeti za Serikali iliyo wazi na inayowajibika kwa umma.

Bajeti ni chombo muhimu ambacho Serikali zinatumia kutekeleza malengo ya kuondoa umasikini, kutoa huduma muhimu kama elimu na afya na kuwekeza kwenye mustakabali wa taifa. Mara hotuba za kisiasa zinapomalizika  kinachobaki kutiliwa maanani ni jinsi Serikali inavyotumia fedha kutekeleza ahadi na vipaumbele.

Mashirika yaliyo kiini cha mchakato huu yanafanya kazi katika nchi na mazingira tofauti na mambo anuwai lakini uzoefu wao wa pamoja unaonesha kuhabarisha na kuhusisha taasisi za kiraia na umma kunaweza kuboresha maamuzi ya kibajeti na matokeo yake, na kwa kufanya hivyo maisha ya raia yakaboreshwa.

Mchakato wa kidunia wa taasisi za kiraia wa Uwazi wa Bajeti, Uwajibikaji na Ushiriki una maono ya kuwa na mifumo ya fedha za umma ambayo inawezesha kupatikana kwa urahisi taarifa za bajeti, kutoa nafasi kwa raia na taasisi za kiraia kushiriki katika maamuzi yanayohusu bajeti, kufuatilia mchakato, na kuwapo taasisi zenye uwezo wa kuiuliza Serikali maswali namna inavyokusanya na kutumia fedha za umma.

Kubadili Fursa kuwa Halisia

Ujio wa harakati hizi unapata msukumo sasa kutokana na matukio makubwa ambayo yanatoa fursa kwa Serikali kujipima na kuboresha namna zinavyofanya kazi, ikijumuisha jinsi zinatumia fedha za umma kutatua changamoto muhimu za watu wao. Matukio ya kustaajabisha zaidi ni mapinduzi ya Arabuni ambayo yameweka fursa ya kipekee kwa Serikali za kidemokrasia na zinazojali hali halisi katika ukanda huo na pia kuziamsha usingizini Serikali nyingine kandamizi kwingineko duniani. Hata hivyo kutumia fursa ya mapinduzi haya kupata Serikali zenye kutimiza majukumu yake kwa uhakika na umakini si swala lelemama na linategemea kuwapo kwa taasisi na mifumo madhubuti, ikiwemo mifumo ya uwazi na wajibikaji ya kibajeti ambayo inawashirikisha raia.

Zipo pia juhudi nyingine za kimataifa zinazojumuisha wadau mbalimbali ambazo zimezinduliwa mwaka jana kuhamasisha uwepo wa Serikali zilizo wazi, za  demokrasia, zinazojali na zinazowajibika. Ya kwanza kati  ya hizi juhudi ni Ushirikiano wa Serikali zilizo Wazi (OGP), ambao unaziunganisha Serikali, taasisi za kiraia na za kibiashara kuhamasisha uwazi, ushirikishwaji wa raia, vita dhidi ya rushwa na matumizi ya teknolojia mpya kuboresha utawala. Ukiongozwa na wenyeviti wenza wawili, rais wa Brazil na rais wa Marekani, OGP unazitaka Serikali kutimiza masharti kadhaa yatakayofanya mifumo yao ya ufanyaji kazi kuwa wazi na inayowajibika.

Jitihada nyingine ya aina hiyo ni jitihada ya kidunia ya uwazi katika masuala ya fedha(kwa kifupisho cha kiingereza (GIFT). GIFT inazitaka Serikali, mashirika ya kimataifa, taasisi za ufuatiliaji, mifuko ya fedha ya kimataifa na taasisi za kiaia kuunda na kuendeleza uwazi katika masuala ya fedha, ushiriki na uwajibikaji duniani kote. Jitihada za GIFT zinahusisha juhudi za kuweka kanuni za kimataifa za uwazi wa bajeti, ushiriki na uwajibikaji; matumizi ya teknolojia kusaidia kazi za bajeti na kutoa vivutio na misaada kwa Serikali zinahitaji kuweka bajeti zao wazi.

Juhudi zote hizi zinatoa matumaini makubwa, lakini bila ushiriki wa taasisi za kiraia zilizoratibiwa vizuri na wenye tashwishwi unaoweza kuunganisha taasisi na vipaumbele na matakwa ya raia wa kawaida na kufanya kazi muhimu ya usimamizi, kuna uwezekano kuwa juhudi nzuri kama OGP na GIFT kutotimiza malengo yao.

Nini kinachofuata?

Mkutano wa mashirika haya hapa Dar es Salaam kuzindua Azimio la Kanuni unaweka jiwe la msingi kwa kila shirika kusaini azimio la kanuni. Azimio hili linaanza na maneno haya:

“Sisi raia na mashirika ya kiraia toka duniani kote, tunaungana katika kuamini kuwa bajeti shirikishi na zilizo wazi ni kiungo muhimu katika kufikia lengo la dunia ambamo watu wote wanafurahia haki zao kamili za kibinadamu—kiraia, kisiasa, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kimazingira.”

Washiriki walikubaliana dhima za pamoja zinazojumuisha kutambua ushiriki wa umma katika kupanga bajeti kama haki ya msingi na uwajibikaji, usawa wa kijamii na ujumuishaji bila ubaguzi, na kuheshimiana. Pia washiriki walitambua mikakati ambayo itatumiwa na mashirika yaliyo katika mchakato huu ili kufanya kazi na OGP na GIFT na michakato mingine inayohusisha mataifa mengi. Soma zaidi.

 

 

 

Endelea kusoma: GIFT

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri