Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

< iliyopita 1234
23 makala
Sort by: Maoni |

Tanzania: Ushiriki, maandamano na siasa

Benki ya taarifa 5 Jul 2018 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wanapotathmini viashiria mbalimbali vya demokrasia, wananchi wengi wanasema uhuru umepungua katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wananchi wanasema uhuru umepungua kwa vyama vya upinzani kufanya mikutano na kutoa maoni yao (64%), vyombo vya habari kukosoa au kuripoti maovu ya serikali (62%), na makundi yasiyofungamana na upande wowote kupaza sauti zao na kufanya mikutano (58%). Nusu ya wananchi pia wanaona hawana uhuru wa kuonesha mitazamo yao ya kisiasa (54%).

Tanzania: Elimu bora au bora elimu?

Benki ya taarifa 16 May 2018 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Muhtasari huu unawasilisha maoni ya wananchi kwenye na masuala yanayohusiana na sera ya elimu. Utafiti huu umebaini kwamba ni wazazi wachache sana huzingatia ada nafuu (6%) na umbali wa shule (18%) wakati wa kuchagua shule za sekondari kwa ajili ya watoto wao. Badala yake wazazi wengi huzingatia zaidi viwango vya juu vya ufaulu wa shule husika (asilimia 72)

Tanzania: Siyo kwa kiasi hicho?

Benki ya taarifa 28 Mar 2018 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Muhtasari huu umebeba takwimu zinazohusu mitazamo na uzoefu wa wananchi kuhusu upatikanaji wa habari na mijadala. Unaripoti kuwa wananchi 7 kati ya 10 wanasema taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma ni mali ya umma (70%, juu zaidi kutoka 60% mwaka 2015); na wananchi 9 kati ya 10 wanasema wananchi wa kawaida wapate taarifa zinazomilikiwa na mamlaka za umma (86%, juu zaidi kutoka 77% mwaka 2015) na kwamba kwa kuwapa wananchi uwezo wa kupata taarifa kunaweza kupunguza rushwa (86%, juu zaidi kutoka 80% mwaka 2015).

Tanzania: Hawashikiki?

Benki ya taarifa 21 Nov 2017 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Muhtasari huu umebeba takwimu zinazohusu mitazamo na uzoefu wa wananchi kuhusu rushwa na maoni yao juu ya namna ya kushughulikia vizuri tatizo hilo. Mara ngapi wanakutana na vitendo vya rushwa serikalini ama kwenye taasisi nyingine? Je, wanafahamu kwa kiwango gani kuhusu kesi za tuhuma za rushwa zilizotawala vichwa vya habari miaka ya hivi karibuni?

Tanzania: Zege imelala?

Benki ya taarifa 18 Oct 2017 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Maoni ya Watanzania kuhusu kukwama kwa mchakato wa marekebisho ya katiba. Wananchi wamegawanyika kwenye baadhi ya hatua za uwajibikaji zilizopendekezwa ikiwemo kuzuia viongozi na watumishi wa umma kuwa na akaunti nje ya nchi (asilimia 52 wanaunga mkono), kuwepo kwa ukomo wa ubunge (asilimia 52 wanaunga mkono) na kuweka kanuni za uwazi na uwajibikaji kuwa sehemu ya tunu za taifa (asilimia 48 wanaunga mkono).

Hapa Usalama Tu

Benki ya taarifa 27 Jul 2017 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Kuna mtazamo wa jumla miongoni mwa wananchi kuwa usalama nchini umeimarika katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita kama inavyooneshwa na zaidi ya nusu ya wananchi hao (asilimia 53).

Matarajio na matokeo

Benki ya taarifa 15 Jun 2017 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Muhtasari huu umebeba maoni ya wananchi juu ya masuala ya kisiasa. Kwa mtazamo wao, ni tati zo gani kuu linaloikabili nchi kwa sasa? Je, tati zo hilo limebadilika ukilinganisha na miaka iliyopita? Je, wananchi wanauonaje utendaji wa viongozi wao, akiwemo Rais? Na je, kuna mabadiliko yoyote kati ka kukubalika kwa vyama mbalimbali vya siasa kati ka kipindi cha miaka michache iliyopita?

< iliyopita 1234
23 makala
Sort by: Maoni |