Twaweza.org

Uwazi

Soma machapisho yaliyotolewa na Uwazi na kusambazwa kama nakala za kawaida na nakala za mtandaoni.

Sort by: Maoni |

Mwangaza: wananchi na haki ya kupata habari

Ingawa sheria inaipa mamlaka serikali kulifungia gazeti bila kuhojiwa, asilimia 91 ya wananchi wanasema kabla ya gazeti kufungiwa suala hilo lijadiliwe kwanza mahakamani.

Usalama Wetu? Maoni ya wananchi juu ya usalama na haki

Wananchi watatu kati ya kumi (30%) wameshakukumbana na wizi ndani ya kipindi cha mwaka jana. Kwa ujumla, nusu ya Watanzania wote wamewahi kuibiwa. Matokeo ya Sauti za Wananchi kuhusu usalama na sheria.

Kuelekea Kura ya Maoni: Maoni ya Watanzania kuhusu Katiba Inayopendekezwa

Wakati kura ya maoni inakaribia, wananchi wamejigawa katikati. Zaidi ya nusu yao (asilimia 52) wanasema wataunga mkono Katiba Inayopendekezwa.

Tanzania ifikapo mwaka 2025: Je, Watanzania wana matarajio gani na maisha yao ya baadaye?

Zaidi ya nusu ya wananchi (54%) wanafikiri kuwa maisha yao yatakuwa bora zaidi ifikapo mwaka 2025. Huu ndio mtazamo wa wananchi wakio katika makundi yote- vijana kwa wazee, wanaume kwa wanawake, na wakazi wa vijijini na mijini.

Tanzania kuelekea 2015: Maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa

Mwananchi mmoja kati ya watatu (33%) Tanzania Bara hajui ni nani atayekuwa chaguo lake la Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hakuna mgombea hata mmoja anayependwa na wapiga kura kwa zaidi ya 15%.

Kulinda haki za kila mtu: Maoni ya wananchi juu ya ulemavu

Karibu nusu ya wananchi (46%) wameripoti kuwahi kushuhudia ubaguzi dhidi ya watu wenye ulemavu katika ajira. Wakati huo huo, ni wananchi wawili tu kati ya kumi (17%) waliokiri kufahamu asasi/mashirika yanayotoa upendeleo kwenye suala la kuwaajiri watu wenye ulemavu.

Hima tujenge nyumba moja! Watanzania wana maoni gani kuhusu Jumuiya ya Afrika Mashariki

Wananchi wanane kati ya kumi (80%) wanafikiri kuwa Tanzania inapaswa kubakia ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Aidha, wananchi tisa kati ya kumi (85%) wanakubali uwepo wa ushirikiano mkubwa zaidi na Kenya na Uganda.
Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri