Twaweza.org

Katika vyombo vya habari

Hapa utapata taarifa au habari zilizochapishwa au kutangazwa katika vyombo vya habari mbalimbali.

Sort by: Maoni |

Matokeo ya mtihani wa kumaliza shule ya msingi Kenya yathibitisha matokeo ya Uwezo

Gazeti la Star la Kenya limeonyesha kuwa viongozi na wakazi wa Mkoa wa Pwani wanatakiwa kukabili changamoto za elimu. Mkoa huu ni wa mwisho katika matokeo ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Kenya kwa 2011. Matokeo haya yanathibitisha utafiti wa Uwezo- Kenya 2011 juu ya tathmini ya Ujifunzaji. Mwandishi wa maoni magazetini anashauri kwamba viongozi waanze kushughulikia utafiti uliofanywa na Uwezo Kenya kama njia moja wapo ya kuboresha elimu katika wilaya sita za Mkoa wa Pwani.

Rekebisheni kiwango duni cha elimu wafadhili waiambia Serikali

Gazeti la The Citizen la Tanzania linaripoti kuwa wafadhili wameichagiza Serikali kutilia maanani ubora wa elimu. Gazeti linamnukuu Bw. Robert Orr, balozi wa Canada nchini Tanzania, katika mkutano wa tathmini ya sekta ya elimu jijini Dar es Salaam, akisema kuwa haitoshi kugawa walimu na vitabu mashuleni. Ni muhimu pia kuhakikisha walimu wamo madarasani na wana moyo wa kufundisha.

Elimu kwa watoto ni muhimu kwa muskabali wa Uganda

Uwezo imenukuliwa katika makala ya IRIN (Integrated Regional Information Networks) iliyochapwa na allheadlinenews.com. Mwandishi anatumia matokeo ya Uwezo toka kwenye Ripoti ya Upimaji wa Kujifunza 2010 kuonesha jinsi shule za vijijini za Uganda zilivyo nyuma katika kiwango cha elimu. Huko wilaya ya Kotido, Karamoja 13% tu ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa elimu ya msingi ndio wanaweza kufanya hesabu za kiwango cha darasa lao.

Ahadi za Sera Bora: Je Serikali ya Uganda ina nia ya dhati

Gazeti la kila wiki la Uganda, The Independent, na la kila siku la New Vision yote yanachapisha maoni ya uchambuzi yalioandikwa na Morrison Rwakakamba, Meneja wa Twaweza Uganda.

Katika uchambuzi huo, Morrison anaonesha mashaka yake kuhusu utashi wa Serikali ya Uganda kutekeleza ahadi zake za sera za kuwa wazi kwa raia wake. Uganda inazo sifa za kuingia kwenye Ushirikiano wa Serikali zilizo Wazi(OGP) lakini haikufanya hivyo OGP ilipozinduliwa Septemba 2011 huko New York. Zaidi ya hayo, mwandishi anadai kuwa Serikali haijatimiza ahadi ya uwazi na uwajibikaji katika udhibiti wa fedha za umma, ahadi ambazo ni pamoja na uwazi katika kutoa misamaha ya kodi na kutoa machapisho ya hesabu za Serikali.

Mkuu wa Wilaya: wanafunzi 3000 hawajui kusoma Iringa

Kwanza Jamii, gazeti jipya la Iringa, linamnukuu Mkuu wa Wilaya hiyo akisema zaidi ya wanafunzi 3000 wa darasa la tatu hadi la saba hawajui kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza. Utambuzi huu, unaosemwa na kiongozi wa juu wa Serikali wilayani, unaakisi matokeo ya Ripoti ya Uwezo ya Upimaji wa Kujifunza 2011. Mkuu wa wilaya anawashauri wazazi, wanafunzi na waalimu kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza idadi ya wanafunzi wasioelimika.

Vuguvugu kuchagiza ongezeko la fedha za elimu lashika kasi Kenya

The Standard la Kenya, linaripoti kuwa Chama cha Wakuu wa Shule za Sekondari na kile cha Wakuu wa Shule za Msingi vinataka ruzuku ya elimu kwa mwanafunzi iongezeke toka Ksh 10,265 hadi 20,000 kwa sekondari na toka Ksh 1,020 hadi Ksh 7,250 kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi. Viwango vya sasa viliwekwa mwaka 2003 wakati Kenya ilipoanzisha mpango wa elimu ya sekondari ya kutwa bure. Wakuu wa shule wanatoa rai kuwa tangu wakati huo bei za bidhaa zimeongezeka maradufu.

Vyombo vya habari Afrika Mashariki vyaandika kuhusu Ushirikiano wa Serikali Zilizo Uwazi

Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri