Twaweza.org

Uwazi

Soma machapisho yaliyotolewa na Uwazi na kusambazwa kama nakala za kawaida na nakala za mtandaoni.

Sort by: Maoni |

Je, juhudi za serikali zimesaidia vita dhidi ya rushwa? Mtazamo wa watu kuhusu rushwa nchini Tanzania

Wananchi wanaiona rushwa katika sekta zote za huduma za Serikali kama kitu cha kawaida kabisa. Sekta zinazoongoza kwa rushwa ni pamoja na polisi (94%) na siasa (91%).

Nini kinaendelea kwenye shule zetu? Wananchi watafakari juu ya hali ya elimu

Mwananchi 1 tu kati ya 10 ndiye anayefikiri kuwa watoto wengi wanaomaliza darasa la 2 wana uwezo wa kusoma na kufanya hisabati wa darasa hilo hilo (ngazi ya darasa la 2). Mbaya zaidi, wananchi 3 tu kati ya 10 (31%) wanafikiri kuwa watoto hawa wanapaswa kuwa na uwezo wa kusoma na kuhesabu kwenye ngazi yao.

Kusimamia Maliasili: wananchi wanasemaje?

Wananchi wanne kati ya watano wanaamini kuwa mafuta na gesi yatawanufaisha wao, watoto wao na nchi yao kwa ujumla. Wakati huo huo, wananchi wanne kati ya kumi (37%) wanaamini kuwa viongozi wa Serikali na matajiri ndio wataofaidika zaidi.

Je, vituo vya afya vipo kwa ajili ya kuwahudumia watu?

Ni mtu 1 tu kati ya watu 20 (6%) mwenye umri zaidi ya miaka 60 na ni mtoto 1 kati ya 5 (18%) mwenye umri chini ya miaka mitano ambao hupata huduma na matibabu bure katika vituo vya afya. Sera ya Nchli inasema kuwa huduma kwa wagonjwa wa nje kutoka makundi haya mawili ni bure, lakini wananchi wanasema kuwa wanatozwa pesa.

Fedha zinamiminika, maji kiduchu

Bajeti kwa ajili ya kuboresha huduma ya sekta ya maji imeongezeka karibu mara tano kati ya mwaka 1999/2000 na mwaka 2011/2012, lakini hakujawa na ongezeko la tarakimu wala ubora wa upatikanaji wa huduma ya maji safi katika kipindi hicho.

Kurasimu Sheria Mama ya Nchi

Zaidi ya theluthi moja (36%) ya Watanzania Bara wameshiriki katika marekebisho ya katiba kupitia mikutano ya jamii, SMS, mahojiano, barua na barua pepe.Pia, karibu nusu ya Watanzania Bara wanaweza kuelezea Katiba ni nini.

Wananchi, redio, mbao za matangazo: Mahitaji na upatikanaji taarifa nchini Tanzania

Uamuzi wa Serikali wa hivi karibuni wa kuhama kuelekea kwenye urushaji matangazo ya televisheni kwa njia za digitali na kodi mpya ya kadi za SIM vimeibua mjadala wa kitaifa kuhusu upatikanaji wa taarifa na mawasiliano. Sauti za Wananchi ilitaka kujua ni njia zipi za awali Watanzania huzitumia ili kupata taarifa na ni za aina gani; endapo wananchi walikuwa wanawajua wanasiasa na sera; na kama kuna mahitaji ya taarifa kutoka Serikalini.
Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri