Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

1234
23 makala
Sort by: Maoni |

Machoni mwa umma

Benki ya taarifa 15 Jun 2015 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Asilimia 84 ya wananchi wanaunga mkono kifungu cha sheria ya upatikanaji wa habari. Wananchi nane kati ya kumi wanaamini taarifa za mamlaka za umma zinapaswa kupatikana kwa wananchi wa kawaida (77%).

Kuelekea Kura ya Maoni

Benki ya taarifa 1 Apr 2015 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wakati kura ya maoni inakaribia, wananchi wamejigawa katikati. Zaidi ya nusu yao (asilimia 52) wanasema wataunga mkono Katiba Inayopendekezwa. Lakini mwananchi mmoja kati ya wanne (asilimia 26), sawa na nusu ya wanao tayarajia kuiunga mkono katiba, wanasema wataipinga. Mwananchi mmoja kati ya watano (asilimia 22) bado hajamua.

Walezi wa uwajibikaji

Benki ya taarifa 24 Feb 2015 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi saba kati ya kumi (69%) wanasema rushwa zilizoripotiwa kwenye ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni upotevu wa fedha zao (za umma).

Tanzania kuelekea 2015

Benki ya taarifa 11 Nov 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Mwananchi mmoja kati ya watatu (33%) Tanzania Bara hajui ni nani atayekuwa chaguo lake la Rais kwenye uchaguzi mkuu ujao. Hakuna mgombea hata mmoja anayependwa na wapiga kura kwa zaidi ya 15%. Maoni na matakwa ya wananchi juu ya uongozi wa kisiasa.

Wananchi wana uchu wa mabadiliko

Benki ya taarifa 1 Sep 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi walio wengi (70%) wanaripoti kuwa sauti zao hazisikiki katika maamuzi ya Serikali.Licha ya mwingiliano mdogo ulio wazi kati ya wananchi na mifumo rasmi ya serikali, wananchi 6 kati ya 10 (58%) wanaripoti kuwa wamewahi kushuhudia wananchi wakipeleka malalamiko kwa viongozi ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Je, juhudi za serikali zimesaidia vita dhidi ya rushwa?

Benki ya taarifa 4 Aug 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi wanaiona rushwa katika sekta zote za huduma za Serikali kama kitu cha kawaida kabisa. Sekta zinazoongoza kwa rushwa ni pamoja na polisi (94%), siasa (91%), afya (82%), kodi (80%) , ardhi (79%), elimu (70%), serikali za mitaa (68%) na maji (56%). Pia wananchi 50% wanaona mashirika yasiyo ya kiserikali nayo yanajihusisha na rushwa. Sekta pekee zinazoonekana kuwa na viwango vya rushwa chini ya 50% ni zile za biashara pamoja na mashirika ya dini.

Je, Watanzania wanaionaje katiba?

Benki ya taarifa 22 Apr 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Mjadala katika Bunge la Katiba umejaa na ubishi na mgawanyiko, lakini Watanzania wameungana kutaka katiba yenye uwajibikaji zaidi kwa viongozi wa umma na mfumo wa utawala wenye uwazi zaidi.

1234
23 makala
Sort by: Maoni |