Twaweza.org

Machapisho

Twaweza kupitia kituo chake cha habari,Uwazi inatoa machapisho mbalimbali kwa wananchi wa Afrika Mashariki na ulimwengu mzima ili waweze kujipatia taarifa za kuaminika na pasipo na gharama. Taarifa hizi ni mkusanyiko wa takwimu, ripoti, tafiti mbalimbaliza kisayansi na vielelezo vya sekta lengwa za Twaweza. Tutajitahidi kadiri iwezekanavyo kuzitoa katika lugha nyepesi . Tembelea kurasa hii kila wakati ujipatie mambo mapya.

Sort by: Maoni |

Hali Halisi: Maoni ya wananchi juu ya elimu bila malipo ya ada.

Maoni ya wananchi kuhusu hali ya elimu nchini Tanzania ndani ya mwaka mmoja uliopita; hasa juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha elimu kwa kuongeza madawati, elimu bila malipo na ruzuku zinazotumwa moja kwa moja mashuleni.

Demokrasia, udikteta na maandamano: Wananchi wanasemaje?

Demokrasia na uhuru wa kutoa maoni ni vitu viwili vinavyothaminiwa sana na wananchi. Asilimia 95 ya wananchi wanauthamini uwezo wa kuikosoa serikali pale wanapoona imekosea. Na asilimia 69 wanakubali kuwa demokrasia ni mfumo bora wa utawala.

Rais wa watu? Tathmini na matarajio ya wananchi kwa serikali ya awamu ya tano

Maoni ya wananchi katika miezi ya awali ya uongozi wa Rais Magufuli. Je, ni vitendo gani vya Rais ambavyo vimejipatia umaarufu mkubwa? Na je, wananchi wanaona mabadiliko yoyote kwenye utendaji wa serikali?

Je, watoto wetu wanajifunza?

Baadhi ya watoto wa darasa la 7 hawawezi kufanya majaribio ya darasa la 2.

Nyota njema huonekana asubuhi: Maoni ya wananchi kuhusu huduma za afya

Wananchi wanao ufahamu kuhusu ubora na upatikanaji wa huduma za afya pamoja na wahudumu wake ambao umeongezeka tangu 2015 kutokana na ripoti za wananchi.

Masuala ya Muungano: Maoni ya wananchi kuhusu kinachoendelea Zanzibar

Nusu ya wananchi wa Tanzania Bara hawafahamu kilichojiri Zanzibar tangu uchaguzi mkuu.

#BungeLive

Watanzania walio wengi (79%) hawakubaliani na maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kupitia runinga na redio.
Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri