Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

1234 ifuatayo >
23 makala
Sort by: Maoni |

Kurasimu Sheria Mama ya Nchi

Benki ya taarifa 4 Dec 2013 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Zaidi ya theluthi moja (36%) ya Watanzania Bara wameshiriki katika marekebisho ya katiba kupitia mikutano ya jamii, SMS, mahojiano, barua na barua pepe. Idadi kubwa walishiriki kupitia mikutano ya jamii iliyoandaliwa na Tume ya Kurekebisha Katiba (CRC). Pia, karibu nusu ya Watanzania Bara wanaweza kuelezea Katiba ni nini.

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika utafiti uitwao: Kurasimu Sheria Mama ya Nchi: Tafakari ya Wananchi wa Tanzania Bara kuhusu Rasimu ya Katiba. Msingi wa utafiti huu mfupi ni taarifa kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wenye uwakilishi kitaifa, uliotumia simu ya mkononi, ngazi ya kaya katika Tanzania Bara.

Sauti za Wananchi, Upatikanaji taarifa

Benki ya taarifa 7 Aug 2013 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Karibu wananchi wote (97%) wanatambua picha ya Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ila ni wachache wanaoweza kuelezea kuhusu sera ya MKUKUTA (7%) au Visheni ya Maendeleo ya 2025 (5%). Sera maarufu ya kitaifa inayojulikana zaidi ni Kilimo Kwanza ambapo walau watu 3 kati ya 10 (33%) wamewahi kuisikia na wanaweza hata kuielezea. Baada ya Rais Kikwete, asilimia iliyo chini ya nusu (48%) ya wahojiwa, wanaweza kumtambua Waziri Mkuu Mizengo Pinda. Wakati huo huo, karibia nusu (42%) ya wananchi wangependa Serikali iweke hadharani data na taarifa nyingi zaidi.

1234 ifuatayo >
23 makala
Sort by: Maoni |