Twaweza.org

Matangazo

Pata habari mpya mpya na matangazo mbalimbali hapa:

Sort by: Maoni |

Viongozi wakutana kuadhimisha mwaka mmoja wa Ushirikiano na Serikali Wazi

Maadhimisho ya mwaka mmoja ya Serikali kwa Uwazi (unaofahamika kama OGP) yalifanyika jijini New York wakati Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ukiendelea.

Zabuni za kuendesha taftishi wananchi kwa simu ya mkononi inatangazwa

Teknolojia ya simu ina uzuri katika kukusanya taarifa kwa bei nafuu, na kwa njia rahisi na sikivu zaidi katika kubadilisha taarifa kwa hitaji la huduma za ufuatiliaji, utoaji huduma na uwajibikaji. Kwa kutumia wazo hili, Uwazi iliyopo Twaweza wanataka kutekeleza taftishi kwa kutumia masafa ya mtandao wa simu za mikononi. Kaya zitachaguliwa kuwakilisha taifa zima kwa kuanza na nyumba 1500 Tanzania. Taarifa zitakazokusanywa kwa njia hii itaujuza umma na kuibua mjadala wenye mashiko kuhusu sera mbalimbali za umma katika Tanzania. Taftishi ya Wananchi inakaribisha maombi toka kampuni za utafiti ili kufanya kazi hii. Soma zaidi.

Nafasi mpya za kazi zinapatikana Tanzania, Kenya na Uganda!

Twaweza inakua! Bofya kwenye tovuti yetu: Je unapenda kile tunachoamini na kile tunachofanyia kazi? Je una shauku na mshawasha wa kujifunza? Je wewe ni mbunifu, unajaribu mambo mapya kwa uangalifu na una kawaida ya kutekeleza mambo? Ungependa kushiriki kuleta mabadiliko Afrika Mashariki? Basi, unafanana nasi! Tazama ukurasa wetu wa nafasi za kazi (kwa Kiingereza).

Wekeni bajeti wazi wa umma, Serikali zaambiwa

Tarehe 18 Novemba 2011 karibu makundi 100 ya taasisi za kiraia toka nchi nyingi duniani na mashirika 12 ya kimataifa, yakijumuisha Ushirikiano wa Kimataifa wa Uwazi wa Bajeti, Greenpeace na Kampeni ya ONE, walizindua juhudi za dunia nzima kuchangiza bajeti za Serikali kuwa wazi, shirikishi na zenye kuakisi uwajibikaji. Juhudi hii inajikita katika kujenga muungano wenye nguvu utakaofanya kazi toka mashinani, kitaifa na kimataifa kuhamasisha michakato ya bajeti za Serikali iliyo wazi na inayowajibika kwa umma.

Bajeti ni chombo muhimu ambacho Serikali zinatumia kutekeleza malengo ya kuondoa umasikini, kutoa huduma muhimu kama elimu na afya na kuwekeza kwenye mustakabali wa taifa. Mara hotuba za kisiasa zinapomalizika kinachobaki kutiliwa maanani ni jinsi Serikali inavyotumia fedha kutekeleza ahadi na vipaumbele.

Sasa ShujaazFM ipo YouTube

ShujaazFM, mradi wa mawasiliano nchini Kenya na mbia wa Twaweza sasa unarusha matangazo yake kwenye mtandao wa picha za video wa YouTube. Chaneli ya YouTube ya inaongeza kitu kingine bora kwenye mkusanyiko wa mitandao jamii ya ShujaazFM ambapo awali ilikuwapo kwenye Facebook na Twitter.

Gazeti la vichekesho la ShujaazFM ndio chapicho kubwa zaidi nchini Kenya, kilisambaza zaidi ya nakala 600,000 kila mwezi.

Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi Waanza Kazi Afrika Mashariki

Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi (Open Government Partnership-OGP) ulizinduliwa rasmi jijini New York, 20 Septemba 2011 na Rais Barack Obama. Wawakilishi toka nchi 40 walihudhuria uzinduzi wa OGP, wakiwamo Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, Rais Zuma wa Afrika Kusini, na mawaziri toka Kenya. Kutoka Afrika ni nchi sita tu zilikidhi vigezo vya msingi kujiunga na ushirikiano huu, kati ya hizo, tano zilijiunga na sasa zinaandaa mikakatiya kitaifa ya utekelezaji wa kanuni za Ushirikiano huo.

Kufuatia hayo, Twaweza, kwa kuitikia wito wa Rais Kikwete, imetoa maelezo kuhusu Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi kwa nyakati tatu tofauti kwa maofisa wa juu wa Serikali Ikulu, kwa Makatibu Wakuu na kwa Baraza la Mawaziri. Unaweza kunyonya taarifa za maelezo hayo hapo chini. Katika mikutano hii Rais Kikwete amesisitiza hitaji la kuwa wazi kwa raia katika mambo yanayowagusa, mathalani huduma za msingi na mambo ya fedha za umma. Rais amemteua Waziri wa Utawala Bora, Mathias Chikawe, kuongoza mchakato huo kwa niaba ya Serikali.

Changia mawazo kwenye andiko la mkakati wetu

Sort by: Maoni |

zinazotumwa katika RSS

 

Tafsiri

wanaohusishwa