Twaweza.org

Mpya

Elimu kwa watoto ni muhimu kwa muskabali wa Uganda

Uwezo imenukuliwa katika makala ya IRIN (Integrated Regional Information Networks) iliyochapwa na allheadlinenews.com. Mwandishi anatumia matokeo ya Uwezo toka kwenye Ripoti ya Upimaji wa Kujifunza 2010 kuonesha jinsi shule za vijijini za Uganda zilivyo nyuma katika kiwango cha elimu. Huko wilaya ya Kotido, Karamoja 13%  tu ya wanafunzi wa mwaka wa mwisho wa elimu ya msingi ndio wanaweza kufanya hesabu za kiwango cha darasa lao.

Karamoja ni sehemu ya mkoa wa Kaskazini-mashariki ambao ndio unapona madhara ya miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwe wenyewe. Pamoja na juhudi za Serikali na wabia wa maendeleo kuhimiza wazazi kuandikisha watoto wao na kuwaacha waendelee na masomo watoto wengi wanaacha shule,. Inakadiriwa kuwa 25% ya watoto wanaoandikishwa shule ndio wanaomaliza miaka saba ya elimu ya msingi. Soma zaidi.

 

Endelea kusoma: elimu

Kuhusu mtunzi

unaweza pia kupenda...