Twaweza.org

Mpya

Rekebisheni kiwango duni cha elimu wafadhili waiambia Serikali

Gazeti la The Citizen la Tanzania linaripoti kuwa wafadhili wameichagiza Serikali kutilia maanani ubora wa elimu. Gazeti linamnukuu Bw. Robert Orr, balozi wa Canada nchini Tanzania, katika mkutano wa tathmini ya sekta ya elimu jijini Dar es Salaam, akisema kuwa haitoshi kugawa walimu na vitabu mashuleni. Ni muhimu pia kuhakikisha walimu wamo madarasani na wana moyo wa kufundisha.Kati ya 2007 na 2010 idadi ya wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu imeshuka toka 35.6% hadi 11%. Serikali inafanya upimaji kutambua kiini cha kushuka ufaulu kwenye mitihani ya kidato cha nne mwaka 2010. Ikifanya kazi na wabia wake na kwa kusambaza machapisho, Twaweza imekuwa ikitetea matumizi ya uwezo wa kuelewa kupima kiwango cha elimu, badala ya kujivunia ongezeko la uandikishaji wa wanafunzi kwenye shule za msingi na sekondari.

Kwenye mwaka huu wa fedha Kundi la Wabia wa Maendeleo katika Elimu limechangia 12% ya bajeti ya sekta ya elimu. Soma zaidi.

Endelea kusoma: agency education Tanzania

Kuhusu mtunzi

unaweza pia kupenda...