Twaweza.org

Shule za msingi za Serikali Dar es Salaam:Vyoo vibovu, michezo kidogo.

Uwazi iliyopo Twaweza imetoa muhtasari mpya wa sera unaoripoti kuhusu hali ya huduma za usafi na michezo kwenye shule za msingi za Dar es Salaam. Muhtasari huo unaitwa, “Shule za msingi za Serikali Dar es Salaam:Vyoo vibovu, michezo kidogo.” Watafiti wanaonesha kuwa kwa wastani watoto 90 wanategemea tundu moja la choo kinyume na malengo ya Serikali kuwa wasichana 20 kutumia tundu moja na wavulana 25 kutumia tundu moja.

Muhtasari huo wa utafiti umechapishwa baada ya kukamilika kwa utafiti uliofanyika kwenye sampuli ya shule 40 za Dar es Salaam kati ya mwezi Agosti na Desemba mwaka 2010.

Watafiti wanapendekeza kuwa shule za Serikali zisifunguliwe kwa masomo mara zinapojengwa hadi pale miundombinu ya kutosha ya usafi na michezo imewekwa. Soma matokeo ya utafiti.

Endelea kusoma:

Authors: Uwazi

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri