Sasa ShujaazFM ipo YouTube

ShujaazFM, mradi wa mawasiliano nchini Kenya na mbia wa Twaweza sasa unarusha matangazo yake kwenye mtandao wa picha za video wa YouTube. Chaneli ya YouTube ya inaongeza kitu kingine bora kwenye mkusanyiko wa mitandao jamii ya ShujaazFM ambapo awali ilikuwapo kwenye Facebook na Twitter.
Gazeti la vichekesho la ShujaazFM ndio chapicho kubwa zaidi nchini Kenya, kilisambaza zaidi ya nakala 600,000 kila mwezi. Kipindi chake cha redio kinarushwa hewani na vituo 20 na maelfu ya mashabiki wanawasiliana kupitia Facebook na Twitter. Washabiki pia wanawasiliana na waigizaji kupitia ujumbe mfupi wa simu na sasa, wanaweza kuwaona nyota wao maarufu kwenye YouTube.
Masuala kuhusu kuongeza kipato na kuepuka shari mitaani yanajadiliwa kwa dakika 5-7 kwenye vipindi vya redio kila siku. Vijana wanapata fursa kuongea, kuwasiliana na kupata taarifa zinazowahusu. Waigizaji wanawatia moyo wasikilizaji kuboresha maisha yao. Mada ni pamoja na mawazo ya kupata fedha na kujiepusha na shari. Fuatilia ShujaazFM YouTube
Endelea kusoma: Kenya media shujaazFM youth
unaweza pia kupenda...
- Zabuni za kuendesha taftishi wananchi kwa simu ya mkononi inatangazwa (20 Jan 2012)
- Nafasi mpya za kazi zinapatikana Tanzania, Kenya na Uganda! (21 Dec 2011)
- Wekeni bajeti wazi wa umma, Serikali zaambiwa (21 Nov 2011)
- Ushirikiano wa Serikali Zilizo Wazi Waanza Kazi Afrika Mashariki (25 Oct 2011)
- Wananchi Wazungumza kuhusu Matokeo ya Kidato cha Nne (14 May 2013)
- Sauti za Wananchi (14 Feb 2013)
- Mpango wa KiuFunza - Kiu ya Kujifunza - Wazinduliwa (2 Feb 2013)

