Twaweza.org

Wakazi wa Dar wanasemaji kuhusu afya?

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na Uwazi iliyoko  Twaweza umebaini matokeo mchanganyiko katika suala la utoaji  wa huduma ya afya kwa wakazi  wa Dar es Salaam.

Muhtasari uitwao  “Wakazi wa Dar wanasemaji kuhusu afya? Huduma za afya na utendaji  jijini Dar es Salaam” umebaini kuwa sera ya serikali ya kutoa kipaumbele katika huduma za afya imefanikiwa sana katika baadhi ya huduma lakini kazi ya ziada inahitajika maeneo mengine . Kwa mfano asilimia 95% ya kaya zilizohojiwa zimesema zinamiliki angalau chanadurua kimoja. Hata hivyo kinyume na mafanikio hayo kwenye upande wa maji safi ya kunywa bado kunalegalega .Karibia asilimia 50 ya kaya zimesema zinakunywa maji yasiyo salama (hayajachemshwa wala kuwekewa dawa).

Tofauti katika matokeo ya utafiti pia imeanishwa na majibu ya maswali kuhusu vifaa vya tiba ya afya. Ingawa huduma ya ushauri inaonekana kuwa ya kiwango sawa katika hospitali za umma na binafsi, kulikuwa na watumiaji wengi zaidi ambao hawakuridhika na huduma kwenye vituo vya serikali kulinganisha na vituo vya afya binafsi. Muda mrefu wa kusubiri na kuenea kwa  rushwa yaweza kuwa mojawapo ya chanzo cha kutoridhika.

Hata hivyo ' Mafanikio ya hivi karibuni katika sekta ya afya Tanzania inawezekana yamefikiwa  kwa njia ya kutatua matatizo mepesi kwanza , kama vile kusambaza vyandarua bure' kulingana na muhtasari. 'Kuleta mafanikio zaidi  inaweza kuwa na changamoto zaidi kwani inahitaji kushughulikia masuala ya ubora wa huduma, ikiwa ni pamoja na utambuzi bora wa magonjwa, kuwahudumia vizuri na kuwajili wagonjwa, na maboresho katika utoaji wa madawa.'
Muhtasari huu unapatikana kwa Kiingereza na Kiswahili.

Endelea kusoma: afya

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri