Twaweza.org

Misamaha ya Kodi Tanzania

Tanzania inatoa misamaha mikubwa ya kodi ikilinganishwa na mapato yanayokusanywa. Hii inaibua maswali kama hali hii ina manufaa katika nchi ambayo inakabiliwa na changamoto kubwa ya kukusanya fedha za kutosha kugharamia Bajeti yake. Uchambuzi wa Uwazi-Twaweza unaonesha kuwa misamaha ya kodi imeongezeka kwa kasi katika kipindi cha pili cha muongo huu (2006-2010) ukilinganisha na kiasi kilichotolewa katika kipindi chake cha kwanza (2001-2005).

Uchambuzi huu, umeotolewa katika muhtasari uitwao Misamaha ya Kodi Tanzania: Je, ni mikubwa sana na kutufanya tuwe tegemezi kwa misaada?, unapendekeza kuwa Tanzania inaweza kukusanya mapato zaidi kama ingetoa misamaha ya kodi kwa uangalifu zaidi. Mwaka 2008/09 na 2009/10, kwa mfano, Serikali haikutimiza lengo lake la mapato kwa wastani wa TZS 453 bilioni kila mwaka. Katika kipidi hicho hicho, misamaha ya kodi iliyotolewa ilikuwa kwa wastani TZS 724 bilioni kwa mwaka. Utafiti kamili unaweza kupakuliwa hapa chini.

Endelea kusoma:

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri