Twaweza.org

Uwezo Tanzania 2011: Watoto wetu bado hawajifunzi

Mwaka uliopita, Uwezo ilifanya utafiti nchi nzima kupata picha halisi ya namna watoto wetu wanavyojifunza katika ngazi ya elimu ya msingi. Zaidi ya watoto 40,000 kutoka kaya 20,000 na wilaya 38 za Tanzania Bara walishiriki kwenye zoezi hilo. Huu ulikuwa ni utafiti mkubwa na wa aina yake nchini. Mwaka mmoja baadae… Nini kimebadilika? Je watoto wetu wanajifunza zaidi?
Kwa mwaka huu wa 2011, Uwezo Tanzania imepanua wigo wake wa kiutafiti kwa kuwapima watoto 128,005 kutoka kaya 76,796 ndani ya wilaya 132. Kigezo kilichotumika ni kilekile ambacho ni kuwapima maelfu ya watoto kwa kutumia majaribio ya ngazi ya Darasa la 2. Unaweza kusoma taarifa hiyo ya kitafiti hapa.

Endelea kusoma: Elimu Tanzania

pakua nyaraka

Tafsiri

unaweza pia kupenda...

 

Tafsiri