Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

< iliyopita 1234
23 makala
Sort by: Maoni |

Je, juhudi za serikali zimesaidia vita dhidi ya rushwa?

Benki ya taarifa 4 Aug 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi wanaiona rushwa katika sekta zote za huduma za Serikali kama kitu cha kawaida kabisa. Sekta zinazoongoza kwa rushwa ni pamoja na polisi (94%), siasa (91%), afya (82%), kodi (80%) , ardhi (79%), elimu (70%), serikali za mitaa (68%) na maji (56%). Pia wananchi 50% wanaona mashirika yasiyo ya kiserikali nayo yanajihusisha na rushwa. Sekta pekee zinazoonekana kuwa na viwango vya rushwa chini ya 50% ni zile za biashara pamoja na mashirika ya dini.

Sema mwananchi, sema

Benki ya taarifa 22 Sep 2015 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Maoni ya wananchi kuhusu siasa na Uchaguzi 2015.

Walezi wa uwajibikaji

Benki ya taarifa 24 Feb 2015 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi saba kati ya kumi (69%) wanasema rushwa zilizoripotiwa kwenye ripoti ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ni upotevu wa fedha zao (za umma).

Kurasimu Sheria Mama ya Nchi

Benki ya taarifa 4 Dec 2013 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Zaidi ya theluthi moja (36%) ya Watanzania Bara wameshiriki katika marekebisho ya katiba kupitia mikutano ya jamii, SMS, mahojiano, barua na barua pepe. Idadi kubwa walishiriki kupitia mikutano ya jamii iliyoandaliwa na Tume ya Kurekebisha Katiba (CRC). Pia, karibu nusu ya Watanzania Bara wanaweza kuelezea Katiba ni nini.

Matokeo haya yalitolewa na Twaweza katika utafiti uitwao: Kurasimu Sheria Mama ya Nchi: Tafakari ya Wananchi wa Tanzania Bara kuhusu Rasimu ya Katiba. Msingi wa utafiti huu mfupi ni taarifa kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wenye uwakilishi kitaifa, uliotumia simu ya mkononi, ngazi ya kaya katika Tanzania Bara.

#BungeLive

Benki ya taarifa 15 Jun 2016 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Watanzania walio wengi (79%) hawakubaliani na maamuzi ya serikali ya kusitisha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge kupitia runinga na redio.

Wananchi wana uchu wa mabadiliko

Benki ya taarifa 1 Sep 2014 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi walio wengi (70%) wanaripoti kuwa sauti zao hazisikiki katika maamuzi ya Serikali.Licha ya mwingiliano mdogo ulio wazi kati ya wananchi na mifumo rasmi ya serikali, wananchi 6 kati ya 10 (58%) wanaripoti kuwa wamewahi kushuhudia wananchi wakipeleka malalamiko kwa viongozi ndani ya kipindi cha miezi 12 iliyopita.

Rais wa watu?

Benki ya taarifa 14 Sep 2016 | Habari, Utawala Bora na Kuchukua hatua

Wananchi wanakubali hatua zinazochukuliwa na serikali mpya, hususani kuhusu uondoaji wa wafanyakazi hewa, sera ya elimu bure na usimamishwaji wa watumishi wa serikali kutokana na makosa mbalimbali. Lakini hawakubaliani na kuzuiwa uagizwaji wa sukari pamoja na bei elekezi ya sukari.

< iliyopita 1234
23 makala
Sort by: Maoni |