Malipo kidogo ndo mchongo
“Katika wilaya ya Ubungo hakuna hata A moja ya hisabati iliyopatikana wakati wa mtihani wa taifa wa kidato cha nne”
Maneno hayo yalitamkwa kwa uchungu na mbunge wa jimbo la Ubungo katika mkoa wa Dar es salaam, ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Profesa Kitila Mkumbo. “Mbali na hayo, ni 2% tu ya wanafunzi waliofuzu vigezo vya kuendelea na hisabati kwa kidato cha tano” akitilia mkazo zaidi siku ya Terehe 18 mwezi Aprili katika uzinduzi wa KiuHisabati – mradi unao hamasisha Kujifunza na kufundisha somo la Hisabati katika jimbo la Ubungo
KiuHisabati inaainisha kwamba kila mwalimu wa hisabati atapokea kitita cha shilingi 100,000 kwa kila mwanafunzi atakayepata alama za daraja A katika somo la hisabati katika mtihani wa mwaka 2021
Kwa Twaweza, KiuHIsabati ni mpango wa kusisimua, kama vile ambavyo tunaamini (Na tunao Ushahidi pia) kwamba motisha zinaweza kuwahamasisha walimu kuwasaidia wanafunzi kuinua kiu yao ya kujifunza. Huu mpango pia unatufanya tujivunie kwa sababu haitakuwa sawa kwa sisi kutowajibika kwa kuleta wazo la kutoa motisha ya ki-fedha na kuipigia chapuo katika nyanja ya elimu nchini Tanzania kwa kupitia majaribio ya KiuFunza (Kifupi cha Kiu ya Kujifunza)
KiuFunza: Kuhamasisha walimu kwa njia ya kuwapima kutokana na matokeo na kuwazawadia – Pesa kwa matokeo
Mwaka 2014, Mtafiti Mwandamizi toka Twaweza, Profesa Mkumbo alichangia ushahidi wa KiuFunza kwa njia ya mahojiano na walimu juu ya uzoefu wao kutokana na mpango wa motisha za ki-fedha. Alitembelea shule 12 kufanya utafiti wa ubora na timu kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam. Ni wazi kabisa jaribio la kujifunza mabadiliko lilimuhamasisha kuanzisha utekelezaji wa huu mpango katika jimbo lake la Ubungo.
“Imetengenezwa kwa mfano wa KiuFunza, mpango wa motisha ya walimu ambao ufanisi wake umethibitishwa kwa kiasi kikubwa, KiuHisabati ina lengo la kuwahamasisha walimu kuboresha ufundishaji wa hisabati na wanafunzi katika kujifunza ikitilia mkazo zaidi katika ufaulu wa mtihani wa taifa” Profesa Mkumbo ambaye amekuwa akishirikiana na Twaweza kwa muda mrefu alisema hayo wakati wa uzinduzi.
Kwa kupitia KiuFunza, kushughulikia matokeo hafifu na juhudi ndogo za walimu, Twaweza inalipa Mwalimu ziada kwa kila mwanafunzi mmoja kutokana na matokeo ya wanafunzi katika shule za msingi. Kulikuwa na majaribio ya aina mbili tofauti katika KiuFunza, yote yakitoa matokeo bora zaidi kuliko ile njia ya kawaida ya kujifunza, na kwa sasa awamu ya tatu inafanyika kwa kushirikiana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Twaweza tunapata msisimko kuona wazo letu linachukuliwa na kufanyiwa kazi katika mipango ya serikali. Pia, tunafurahi kuona kwamba sauti za walimu ambazo ni za mchango chanya kuhusu malipo kwa utendaji zikichukuliwa hatua.
Tunafarijika zaidi kuona kwamba serikali inafanyia kazi ushahidi. Wakati anashiriki uzinduzi wa KiuHisabati, Waziri wa Nchi, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa, Mheshimiwa Ummy Mwalimu alitangaza kwamba, kuanzia Julai 1 mwaka 2021 Serikali itazindua mpango wa kuboresha matokeo ambao pia utajumuisha kufufua Vituo vya Rasilimali vya Walimu, ili walimu wawe na maeneo ya kujifunza kuhusu mada ngumu na kubadilishana taarifa na uzoefu katika kufundisha somo la hisabati
Sehemu nyingine ya mradi inahusisha kuchapisha na kusambaza vitabu vya hisabati kwa wanafunzi wote nchini ili kwamba kila mmoja awe na kitabu cha kufanyia marejeo, pamoja na kutoa hamasa na kuwatia moyo kusoma somo la hisabati.
Kwa nini KiuFunza?
Twaweza inaamini katika kuwazawadia walimu kutokana na utendaji kwa sababu katika tafiti binafsi umeonyesha kuinua kiwango cha wanafunzi kujifunza. Pia ni njia ya ubunifu kwa shule na wasimamizi wa walimu nchini Tanzania, ambapo walimu wengi wanafanya kazi bila ya kupokea mrejesho au maoni ya kuwatia moyo kutokana na juhudi zao.
KiuFunza ni mpango wa kumlipa mwalimu kutokana na utendaji wake unaolenga katika ujuzi wa kimsingi katika shule za msingi. Mpango unalenga katika kujenga ujuzi wa msingi katika kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto ndani ya miaka mitatu ya awali shuleni – Ujuzi ambao wanauhitaji ili kuhitimu elimu ya msingi kwa mafanikio (tazama chini)
Source: Rise Programme
Kumzawadia mwalimu mmoja mmoja kutokana na mafanikio ya kuboresha matokeo ya kujifunza, hufaidisha watendaji wote muhimu wa shule. Kwanza, walimu wanapokea mrejesho kutokana na juhudi na mafanikio yao, katika mfumo wa matokeo ya mitihani na zawadi za kifedha. Walimu wanashukuru kwa hili, katika tafiti kadhaa, zaidi ya asilimia 90 ya walimu walikubaliana na wazo la kutoa mapato ya ziada kutokana na matokeo.
Mbili, wanafunzi na wazazi wao wanafaidika kutokana na kuongezeka kwa ari ya kufundisha na umakini wa walimu. Walimu wao wanalenga zaidi katika kuinua kiwango cha uwezo wa kusoma na kuandika kwa sababu matokeo yake yanaunganishwa moja kwa moja na malipo ya kifedha
Tatu, kwa waziri na wadau wengine wenye mamlaka, malipo ya utendaji kwa walimu yana mvuto kwa jinsi yanavyoboresha marejesho katika elimu hasa kwenye mishahara ya walimu, vitabu na majengo ya shule. Mwisho, malipo kutokana na juhudi ya mwalimu yanatoa nafasi ya kuvutia walimu wengi katika sekta ya hesabu.
Tuko wapi sasa?
Twaweza imetekeleza matoleo tofauti ya KiuFunza ndani ya Tanzania kuanzia mwaka 2013 na tumeyaboresha zaidi ili kufikia aina tuliyonayo sasa. Ushahidi wa majaribio kutoka KiuFunza yanaonesha kwamba motisha ndogo ndogo kwa walimu hupelekea mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na ni kwa gharama nafuu. Mradi unatoa miezi 3 – 4 ya kujifunza zaidi kwa kutumia ziada ambayo ni sawa na nusu ya mshahara wa mwalimu. Katika kuongezea, Utoaji wa motisha za kifedha kwa watendaji wa KiuFunza unapelekea kuwa na matokeo chanya katika nyanja ya elimu kuliko mfumo wa kawaida wa uwekezaji katika elimu (Vitabu, Mishahara; Tazama ushahidi wa KiuFunza 1 na 2 (www.twaweza.org) Na mradi huu ni mashuhuru zaidi kwa walimu wakuu na walimu wa kawaida
Kutokana na haya matokeo, waziri wa TAMISEMI ameiomba Twaweza kusaidia katika kubuni toleo ambalo linaweza kufanyiwa kazi la KiuFunza: Mfumo rahisi wa kutoa motisha kwa walimu ambao utawapa motisha ya kifedha walimu wa darasa la 1, 2 na la 3 kutokana na umahiri utakaooneshwa na wanafunzi wao. Maombi haya yametokana na jaribio la pamoja ambalo limefanyika kwa kushirikisha Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Wizara ya Elimu Sayansi na Utamaduni, na Twaweza. Jaribio hili lilifanyika katika shule 100 za umma katika mikoa sita nchini Tanzania.
Timu za Twaweza na Wizara ya Elimu, Wakaguzi wa Elimu walitekeleza mpango/mradi wa kiufunza kwa mwaka 2019-2020. Motisha kwa walimu zililipwa mwezi Februari 2021 kwa ufaulu wa wanafunzi uliopimwa mwisho wa mwaka 2020. Kama ilivyoahidiwa kiasi cha shilingi milioni 170 za kitanzania kililipwa kwa walimu wa somo la hisabati. Shilingi milioni 34 kwa wakuu wa shule, na shilingi milioni 54 kama nyongeza kwa ajili ya kuboresha miundo mbinu ya shule. Malipo kama hayo pia yalifanyika mwezi februari 2020 kwa wanafunzi ambao walipimwa mwisho wa mwaka 2019.
Mlinganisho wa awali wa takwimu katika uingiliaji kati na uendeshaji wa shule unaonyesha kuchochea matokeo mazuri. Takwimu zinaonesha ongezeko kubwa katika kujifunza katika shule zilizo chini ya mradi wa KiuFunza: Motisha kwa walimu hupelekea matokeo mazuri.
Ramani ya Tanzania na sehemu ambazo mradi wa Kiufunza umetekelezwa
Mradi wa kiufunza umeonesha kwa njia mbalimbali kwamba utendaji kazi bora wa walimu unahitaji sana uwekezaji. Unachochea ari ya kujifunza na unaleta thamani ya pesa inayowekezwa ukilinganisha na uwekezaji wa aina nyingine katika elimu. Inatia moyo sana kuona KiuFunza inahamasisha mpango wa kama KiuHisabati. Tunakaribisha maoni haya kuchukuliwa na kutekelezwa kama sera. Mbali na ubunifu wa wazo la kulipa kutokana na matokeo, muundo na utekelezaji wa KiuFunza unahusisha ubunifu mwingi ambao unaweza ukachukuliwa na kufanyiwa kazi katika mfumo wa elimu ili kuinua kiwango cha ufaulu na ufanisi. Tunaendelea kuangalia fursa nyingine za kusambaza haya mawazo pamoja na ushahidi mkubwa ambao tumeukusanya katika kuyathibitisha.
Vyanzo vya Kiufunza:
Inputs, Incentives, and Complementarities in Education: Experimental Evidence from Tanzania