Mpango wa Motisha kwa Walimu unaotekelezwa na Twaweza umesaidia zaidi ya wanafunzi 77,000 katika kuboresha umahiri wao kwenye stadi za Kusoma na Kuhesabu
Wiki hii, walimu kaka shule za msingi 265 kwenye mikoa 11 ya Tanzania wamepokea jumla ya shilingi milioni 401 kwenye akaun zao za benki ikiwa ni mosha kulingana na utendaji wao. Kiwango cha motisha wanayolipwa walimu kinategemea umahiri uliooneshwa na wanafunzi wao katika majaribio ya kusoma na kuhesabu yaliyofanyika mwishoni mwa mwaka wa masomo – 2023.
Read More